UYUMBU ni Jumuia ya Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ambayo ipo katika Kata ya Uyumbu, Tarafa ya Ussoke Wilayani Urambo.
Jumuia ina ukubwa wa eneo la km 838.7. Aidha, Jumuia hii, ina haki ya kutumia raslimali zilizomo ndani ya hifadhi hiyo ambazo ni uwindishaji wa Kitalii, upigaji picha, uwindaji wa kienyeji, uvuvi na uvunaji wa asali na mbao.
Tarehe 19 Novemba, 2012 Waheshimiwa Madiwani Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Haruna Kasele, walifanya ziara ya kwenda kuitembelea Jumuia hii ili kujionea shuguli mbalimbali zinazoendeshwa katika eneo hilo. Ashleymama.com, ilipata bahati ya kuongozana na Waheshimiwa hao katika safari hiyo. Safari ilikua ndefu na ya kuchosha lakini baada ya kufika katika hifadhi hiyo, kamwe sikujuta kwa sababu ya mambo mazuri ya kufurahisha na kupendeza ambayo tuliyakuta kule. Kwakweli, sikuweza kuamini kama eneo lile lipo Urambo lakini ukweli bado unabaki palepale kwamba hifadhi hii ipo Urambo na Watalii kutoka nchi za nje hufika katika hifadhi hii kwa ajili ya kuangalia wanyama na kuwinda. Na pengine nikujuze kuwa, hata mfalme wa jumuia za kiarabu amewahi kufika katika hifadhi hii. It si so wonderful my dear.
Mi nisikumalizie uhondo, ngoja nikushushie picha moja baada ya nyingine ili ili uweze kuona jinsi tulivyokula bata wenzenu.
Wajumbe wakisikiliza maelekezo kutoka kwa wenyeji wa hifadhi
Mandhari ya hifadhi ya WMA
Mto Walla
Waheshimiwa Madiwani wakiwa wametulia .
Waheshimiwa wakibadilishana mawazo
Mkurugenzi wa ABUSAT Bw. Hilal Soud akitoa maelezo kwa Wajumbe
Kushoto ni Mkurugenzi wa Ashleymama.com Bi Teddy Chacha na Kaimu Afisa Elimu (S) Bi. Grace Monge
Mojawapo ya nyumba za kulala wageni wanaofika katika eneo hilo
Mhe. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. H. Kasele akiwa amejiachia kwa raha zake kitandani
Woouw!Nice room
Chinekeee!Mtoto wa kikulya mie, mate yananidondoka kwa uchu wa nyama yarabi
Tobaa mie yarabi, Daaah!
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa ABUSAT Bw. Hilal Soud
Kwakweli, tuliinjoi sana. Hivyo Mtanzania mwenzangu, ukipata nafasi hebu fika mahali hapa ukajionee mwenyewe. Usisubiri kuhadithiwa.
Bahati mbaya ni kwamba, kwa muda tuliokua tumekwenda, ni muda ambao wanyama huwa wamejipumzisha hivyo hatukuona wanyama kivileeee. Ila tuliwaona ila Kamera ya ashleymama.com haikuweza kuwafikia. Walikua mbali halafu walikua wakiona gari wanakimbia. Waoga haoooo.
Asanteni na Karibu tena.
Ashleymama.com.
No comments:
Post a Comment