Friday, January 17, 2014

BABY MADAHA ANASA KATIKA MTEGO WA KUJIUZA.



AMA kweli maovu yanazidi kuongezeka, shetani naye mbioni siku zote kunasa waliyo wake, kauli hizo zote ziko sambamba na staa wa sinema za Kibongo na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Joseph Madaha amenaswa baada kuingia mkenge mtego wa kujiuza, Ijumaa limesheheni.

Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo hujihusisha na biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na kufanya sanaa kuwa kama chambo cha kunasa wanaume.
OFM…

 
Baby Joseph Madah.
AMA kweli maovu yanazidi kuongezeka, shetani naye mbioni siku zote kunasa waliyo wake, kauli hizo zote ziko sambamba na staa wa sinema za Kibongo na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Joseph Madaha amenaswa baada kuingia mkenge mtego wa kujiuza, Ijumaa limesheheni.

Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo hujihusisha na biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na kufanya sanaa kuwa kama chambo cha kunasa wanaume.

OFM MZIGONI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, mwaka jana ilinasa mastaa wawili kwenye mtego wake, mke wa mtu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Mwaka huu, OFM imeanza kazi zake ambapo kwa kuanzia iliamua kumtega Baby Madaha aliyejaa kwenye kumi na nane zake.

Mmoja wa wadau wa OFM alijifanya mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye ni mgeni wa jiji a.k.a Ngosha akijipachika jina la Frank ambapo baadaye katika mazungumzo, Baby Madaha alimbana na kutaka ampatie majina matatu ndipo mwana-OFM Frank (feki) akajipatia jina Frank Michael Lugwisha.

 

ILIKUWAJE?
Mchezo mzima ulianza Januari 13, mwaka majira ya saa 11:52 jioni kwa kuchati kwenye simu ya kiganjani ambapo Baby Madaha aliingia kichwakichwa bila kujua anachati na ‘sumu’ wa OFM kama ifuatavyo;

Frank/OFM: Mambo vipi Baby Madaha? Nilikuwa naomba tuonane.

Baby Madaha: Kuhusu nini?

Frank/OFM: Niwe mkweli, Madaha nimekupenda, nilipofika hapa Dar ndo nikaona nikutafute.

Baby Madaha: Unampendaje mtu usiyemjua?

Frank/OFM: Jamani nakuonaga magazetini na video zako.

Baby Madaha: Safi, so unataka kuniambia nini ambacho sijakisikia?
 Frank/OFM:  Nataka tu-meet (kukutana) Madaha nimetokea kukupenda sana lakini Alhamisi (jana) narudi mkoani Mwanza.

 
Baby Madaha: Huwezi ku-manage kuwa na mimi, baki kuwa shabiki wangu tu.

Frank/OFM: N’take radhi Madaha, kwa nini nisiweze, kikubwa kipi?

Baby Madaha: Huh! Tuma vocha tuone how worth are you? (Tuma vocha tuone utajiri wako).

Frank/OFM: Acha utani bwana, vocha kitu gani, ongea mambo makubwa Madaha

Baby Madaha: Hahaha…yote ninayo-except vocha tajiri.

Frank/OFM: Acha bwana. Vocha ndo kikwazo kwako?

Baby Madaha: Yap! Kama hutaki acha au unadhani natumia wireless kuchati na wewe?

Frank/OFM: Madaha wewe ni mkatili kiasi hicho?

MAMBO YASIMAMA KWA MUDA
Masuala ya kuchati yalisimama kwa muda lakini ilipofika saa 2:22 usiku, mazungumzo yaliendelea ambapo siku iliyofuata Frank wa OFM aliamua kuendelea kumtengenezea mtego ili kujiridhisha kama ni kweli baadhi ya mastaa wa Bongo wanafanya biashara hiyo haramu.

Januari 14, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi, Frank wa OFM alianza tena kuchati na Baby Madaha kama ifuatavyo;


Frank/OFM: Mambo Madaha? Mi Frank

(akaamua kumpigia simu Frank wa OFM, ilikuwa mshtuko kwa Frank kwa sababu hakujipanga kuongea naye kwa hiyo hakupokea simu ya Baby Madaha ambayo ilipigwa saa 6: 30 mchana.

Dakika moja baadaye, Baby Madaha alituma meseji ya kumtoa hofu Frank wa OFM;

Baby Madaha: Frank ‘am calling you in vain uh afraiding of me (Frank nakupigia kwa nia njema unaniogopa?)

Frank/OFM: Sorry nilikuwa tight, naweza kupiga?

Baby Madaha: Yap!

Frank/OFM: Frank wa OFM aliongea na Baby Madaha na kuanza kumchomekea ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kuonesha nia ya kujenga uhusiano huku akimtaka staa huyo kuwa ‘siriaz’ akimuahidi kuwa atakuwa naye na kuwa ajenti wake wa muvi jijini Mwanza.

Baada ya maongezi ya kutongozana kwenye simu, Frank wa OFM alimtumia tena meseji Baby Madaha kama ifuatavyo;


Frank/OFM: Nimefurahi sana kuongea nawe, sijui itakuwaje tukionana?

Baby Madaha: Wait, you I’ll see.

Frank/OFM: Eti ee, nimetokea kukupenda sana.

Baby Madaha: Thanks.

Baada ya hapo Frank wa OFM alimaliza kumtumia ‘sms’ siku hiyo, ilikuwa saa 9:12 alasiri.

Hata hivyo, Frank wa OFM aliamua kumhoji zaidi kupitia sms akitaka kujua hasa akiwa naye hata kwa saa tatu atataka shilingi ngapi? 

Frank/OFM: Sasa hivi nataka kutoka niende ATM kuchukua pesa, sasa hebu kuwa muwazi tu wangu, kuwa na wewe kwa kama saa tatu utakuwa poa nikupe Sh. ngapi? Mtu mzima nisije nikaumbuka si unajua tena kwa staa kama wewe?

Baby Madaha: Milioni 10!

Frank/OFM: Baby usinikomoe, mimi na wewe tuna safari ndefu, kila nikija Dar tutakuwa pamoja.

Baby Madaha: (...anapiga simu lakini Frank wa OFM hapokei).

Baada ya kuona hivyo, Baby Madaha alituma sms hii “Call” (piga).


MAONGEZI YA SIMU
Frank/OFM: Mambo vipi Baby, habari za muda tena?
Baby Madaha: Salama tu, kwani wewe ulikuwa unataka kutoa sh. ngapi ATM?

Frank/OFM: Mimi ndiyo nilikuwa njiani naelekea ATM natoka hapa hotelini nilipofikia nina Shilingi Mil.4 kwa usiku mmoja, hapo vipi?
Baby Madaha: Katoe 5 fresh, sasa benki gani utaenda kutoa wakati benki zote zimeshafungwa na ATM mwisho kutoa ni Mil.1, sasa hapo itakuwaje?

Frank/OFM: Nitatoa kwa ATM, hata hivyo, nina master-card, naweza kutoa Mil.1 hadi mara 5, usijali kwani pesa kitu gani, cha msingi mimi ni kuwa na wewe!

Baby Madaha: Okay, fine unaweza kuja Kijitonyama (Dar) hapa kwenye hoteli ya (anaitaja jina)?

Frank/OFM: Nimefikia hapa hotelini (jina kapuni), sasa kutoka ni vigumu.

Baby Madaha: Okay, poa nitakuja hapo hotelini saa 1:00 usiku.

Frank/OFM: Usijali karibu sana, nakupenda sana Baby Madaha yaani niko tayari kwa lolote, sema unataka nikupe nini? 

Baby Madaha: Hahaha....(anachekaaa) nikija nitakwambia vyote ninavyotaka kwani unafanya biashara gani?
 

Frank/OFM: Nauza nguo, mara nyingi nafuata Jakarta, Indonesia mara kwa mara lakini natumia muda mwingi kufanya kazi zangu Mwanza.

Baby Madaha: Wee Msukuma eti? Mimi mwenyewe Msukuma kwani unadhani jina Madaha ni la nini hilo, mimi mwenyewe Msukuma.

Frank/OFM: Nimefurahi sana kusikia hivyo, unaweza kuongea Kisukuma?

Baby Madaha: Naweza, wewe nisemeshe tu!

Frank/OFM: Nakutogilwe gete Madaha (Frank anaongea Kisukuma kwamba anampenda sana Madaha).

Baby Madaha: Tukuhoya ntondo nduhu tabu (anajibu kwa Kisukuma kuwa hakuna tatizo tutaongea kesho).

Ulipofika muda waliokubaliana na Frank wa OFM, Madaha alisema kuna foleni kubwa hivyo kuna sababu ya kubadilisha hoteli hiyo iliyoko maeneo ya Ubungo alipopanga Frank wa OFM waonane, Baby Madaha akataka wakutane nyingine iliyoko Kijitonyama.

“Siwezi kuja huko, kwanza kuna mifoleni isitoshe ni vizuri ukafika mwenyewe maeneo haya ya hoteli ya… (anataja), ni sehemu nzuri kwangu hivyo kama huna nia mbaya na mimi ni vizuri ukaja maana kesho nasafiri kwenda Kenya kwenye shughuli zangu za muvi, kwa hiyo unaweza kuja wewe tu maeneo haya,” alisema Madaha.

  

Frank aliendelea kumbana kwamba tayari alikuwa ameshaandaa pesa shilingi Mil.5, kama walivyokubaliana lakini asingeweza kubeba mfuko wa fedha wote huo isitoshe ni hoteli ambayo ameizoea kwa muda mrefu.

“Ujue Dar mimi siyo mzoefu, achilia mbali kuogopa kutapeliwa hivyo nakuomba uje kwenye hii hoteli nitafurahi sana dear, nakuomba unielewe ujue nakupenda sana mpenzi wangu Baby Madaha, tulia tuyajenge maisha,” alisema Frank wa OFM.

Msanii huyo alimkomalia Frank wa OFM wakutane siku ya Jumanne usiku ambapo alimwambia pia kuwa amepata dharura anakwenda kumuona mfanyabiashara mwenzake kwenye hoteli moja iliyopo Masaki (jina tunalo) ambapo Baby Madaha alitaka waonane na Frank wa OFM kwenye hoteli hiyohiyo.

“Nimepata dharura sitaweza kuonana na wewe, naenda kumuona mfanyabiashara mwenzangu maeneo ya hoteli…(jina tunalo), tuonane kesho muda wa asubuhi,” alisema Frank.

Baadaye Frank alimjulisha mteja wake kuwa yuko njiani anafuata mzigo bandarini akitoka wataonana na Baby Madaha kesho yake asubuhi ya Jumatano iliyopita, alituma sms hii; 

Baby Madaha: Kuna stage tano in anything, nakupa tatu, coz uko siku ya tatu, denying, bargaining, accepting..... tomorrow if you be still on game, i give you the remained good day, enjoy Mr Frank, ukitoka cargo call me, we meet! 

Frank/OFM: Okay, siku njema nitakutafuta.

 

Baby Madaha: Matajiri wengine hawana maneno kama wewe kwa mfano…(anataja jina la pedeshee mmoja maarufu Dar). Wanatuma pesa na siyo maneno, wee tuma hela (-)-pesa ipo kila sehemu we tuma ndo nitaweza kujiongeza kama nakuja au laa.
Frank/OFM: Nakutumia muda siyo mrefu, usijali.

IJUMAA LAMBANA BABY MADAHA
Hata hivyo, Baby Madaha hakutumiwa pesa alizotaka ili kukamilisha zoezi badala yake, OFM walitua mzigo wa ushahidi kwenye dawati la Ijumaa ambalo lilikuwa na jukumu la kutafuta mzani wa ishu hiyo.

Ijumaa lilipomtafuta Baby Madaha alikiri kuwa kwenye mawasiliano na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Michael Lugisha ambaye alisema alikuwa akifanya naye makubaliano ya kusambaza filamu yake ya The Gal Bladder.

Alipobanwa juu ya makubaliano ya kujiuza kwa mwanaume huyo kwa Sh. milioni 5 alikataa pamoja na kwamba alielezwa kuwa kuna ushahidi wa meseji na sauti.

Alipotakiwa kufika kwenye ofisi za gazeti hili ili kusikilizishwa sauti na kuoneshwa meseji zake, Baby Madaha alisema hawezi kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda nchini Kenya muda mfupi baadaye.
Chanzo: GPL

Kutoka kwa bibi.
Yaani Global, mimi leo naumwa. Jino linaniuma kwelikweli na mdomo wangu umevimba. Hivyo siwezi kusema chochote wala kuinua mkono wangu kutandika mtu. Hata hivyo, mmefanya kazi nzuri sana. Endeleeni kuwanyoosha wote wanoenda tofauti na maadili yetu.
Big Up!

Wednesday, January 15, 2014

Hala, hala wajukuu zangu msije mkaiga fashion hizi.

Wajukuu zangu tafadhali, nawaombeni sana msije mkaiga fashion kama hizi. Maana ntawacharaze bakora. Maana wapo wajukuu zangu wengine akina mama msipitwe. Kesho mtatinga. Marufuku nawambia. Hii ni kinyume kabisa na maadili yetu ya kitanzania. Mambo mengine tunatakiwa tuyaangalie tu na kuyaacha kama yalivyo. Natumai mmenielewa.

                  
                

Sunday, January 12, 2014

AIBU KUBWA!

Wajukuu zangu, hii ni aibu kubwa sana. Dume zima linakosa shughuli za kufanya na kuendekeza chabo. Hata aibu halina. Yaani mimi bibi yenu natamani sana ningekuwepo katika timu hiyo ya OFM ili nimwadabishe kwa bakora huyu mwanaizaya. Ningemtandikaje? Tena naona bakora isingemtosha, ningemn'gata na meno kabisa.Yaani angejuta. Sasa cha ajabu nini ambacho yeye hakijui hadi kuhangaika kujificha uvunguni kusikiliza watu wakila raha zao. Puuh! Aibu yako.



NI aibu kubwa! Mpigachabo maarufu nchini, Andrea Masangu (29) amenaswa akiwa kwenye uvungu wa kitanda akiwapiga chabo wanandoa, Ijumaa Wikienda lina mkasa wote mkononi.

Tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu, ndani ya Gesti ya Riverside, Stendi ya Nyegezi jijini hapa ambapo kijana huyo aliingia kwa kuruhusiwa na mhudumu wa gesti hiyo katika mtego makini uliotegwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na mwishowe kujikuta akiumbuka.

OFM WAPOKEA MASHTAKA
Wiki moja nyuma, mtu mmoja alipiga simu kwa OFM jijini Dar akidai yeye ni msomaji wa Magazeti Pendwa ya Global. Akasema ameamua kupiga simu ili kumshtakia Andrea akidai amekuwa na tabia iliyoota sugu ya kupiga chabo wapenzi wanapokuwa gesti.

“Mimi naitwa…(akataja jina lake), napiga simu kutoka jijini Mwanza. Kuna bwana mmoja anaitwa Andrea, amekuwa na tabia ya kuwachungulia (kuwapiga chabo) wapendanao wanapokuwa gesti.

“Mbaya zaidi, huyu jamaa nasikia huu mtindo anao siku nyingi sana. Amekuwa akienda hata nje ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili hiyo,” alisema mtoa habari huyo.

Akaongeza: “Kuna watu wanasema kuwa hata Tabora, Dodoma wanamjua kwa tabia hiyo. Hebu OFM njooni Mwanza.

Ijumaa Wikienda: Usipate tabu, hukohuko Mwanza kuna OFM wametokea hapa makao makuu. Nawapa namba yako ili mshirikiane.

Mtoa Habari: Mtakuwa mmefanya jambo la maana sana.

KAZI YAANZA
Ndani ya dakika tano tu, OFM waliopo Mwanza wakapewa namba za mnyetishaji wetu, kazi ikaanza.

OFM Mwanza, walimtafuta mtoa habari huyo na kukaa naye meza moja ambapo walipanga mipango.

Miongoni mwa mipango hiyo ilikuwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi jijini Mwanza ambapo maafande walijipanga.

SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, Andrea alikwenda kwenye gesti hiyo na kumuuliza mhudumu kama kuna wateja wa ‘shot’ taimu’ wataingia, akajibiwa wapo njiani.

Akaomba alipe shilingi elfu mbili (2,000) ili atangulie kuingia yeye kwenye chumba ambacho mhudumu huyo atahakikisha anawaingiza wapendanao hao.
OFM WAJULISHWA, WAINGIA
 
OFM walijulishwa kuwa mpiga chabo huyo amewasili na tayari ameingia chini ya kitanda kwenye gesti hiyo, nao wakamchukua OFM mwanamke na kutinga naye sanjari na Polisi wa Dawati la Jinsia Jiji la Mwanza.

OFM WAMCHEZEA MCHEZO
Ndani ya chumba hicho, wapendanao (mke na mume) hao walifikia kitandani. Lakini ili kujiridhisha kama kweli Andrea alikuwa uvunguni, OFM mwanaume alijifanya ameangusha pesa chini, alipoinama kuiokota akamuona kiaina lakini hakuonesha kushtuka.

Ndipo OFM hao ‘wapendanao’ walianza kuchojoa nguo za juu na kuzitupa chini kana kwamba walikuwa tayari ‘mchezoni’ ili kumshawishi Andrea aendelee kuamini na kufurahia dhamira yake chafu.

OFM NJE YA GESTI
Nini kilibaki hapo kama si OFM waliokuwa chumbani kuwajulisha kwa simu wenzao waliokuwa nje na polisi?

Chumba kilivamiwa, Andrea akajikuta yuko chini ya mikono ya sheria akionekana ameingilia faragha.

ETI AKAJITETEA!
Baada ya kutolewa chini ya kitanda, Andrea aliwekwa mtu kati na kuhojiwa kulikoni kuwa mpiga chabo wa kiwango kile?

Andrea alianza kwa kuomba msamaha na kuahidi kuacha kabisa tabia hiyo. Alikiri amekuwa akichungulia watu wengi sana wanaofika katika gesti za jijini Mwanza.

“Jamani nimekoma, ni shetani tu, naacha kabisa mambo haya ‘haki  ya Mungu’ kuanzia leo sifanyi tena. 

“Kweli nimewachungulia watu wengi sana na sijapata faida yoyote, sijui shetani gani aliniingia,” alilalama Andrea na kuongeza kuwa hayupo peke yake bali ana marafiki zake wengi ambao hufanya kama anavyofanya yeye.

Soo hilo liliisha kwa Mshauri Nasaha wa Taasisi ya Farijika, Aisha Mtumwa kumrekebisha kisaikolojia Andrea sambamba na kumpa onyo kwamba akirudia tena atatupwa rumande kwa kosa la kuingilia faragha ya watu.

Chanzo: GPL

WAJUKUU ZANGU, KWELI ZIPO STAILI MBALIMBALI ZA KUTAFUTA RIZIKI LAKINI HII KIBOKO.

Wajukuu zangu, hivi hakuna kabisa njia nyingine ya kujiingizia kipato iusipokuwa hii? Hapana, mimi sikubaliani kabisa na ninyi kwani huku ni kujidhalilisha wenyewe na wanawake wote kwa ujumla. To me, Big Nooo!


Kundi la Khanga Moja la Jijini Dar limepigwa marufuku kukanyaga Mkoani Bukoba kutokana na vitendo vya kifuska walivyovifanya huko.
Kwa mujibu mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina Rubangila aliimbia Xdeejayz  kuwa kundi hilo limeacha laana kubwa sana mkoani humo kiasi cha kutia kinyaa hivyo wananchi mbalimbali wamesema kuwa hata siku moja wasithubutu kutia pua  zao kwenye ardhi hiyo.
 
Chanzo: Lewis Mbonde Blog

UBUNIFU WA HII KEKI UMENICHAFUA. HAKIKA SIJAUPENDA HATA KIDOGO.

Mmh! Mimi bibi yenu nimeishia kuguna tu. Nawaombeni sana wajukuu zangu, msiige keki hii. Ni aibu.

Friday, January 10, 2014

SALON KUTUMIKA KAMA DANGURO KUNA WADHALILISHA WAJUKUU ZANGU. JIHESHIMUNI.


AMA kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine, Ijumaa linaibumburua.

Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM.

Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa uchafu…

Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa uchafu wa aina yake nyuma ya pazia.

Saluni hiyo maarufu kuliko Miji ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yaliyotukuka.

TAARIFA MEZANI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, ikiwa imetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar, Mkuu wa kikosi maalumu cha Mtambo wa Kurekebisha Tabia (MKT) ambacho ni kitengo ndani ya OFM, alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema akitoa ‘tipu’ juu ya ishu hiyo.

Mhudumu baada ya kumpatia dozi mteja.

Mtoa taarifa huyo alieleza malalamiko yake juu ya kero wanayoipata raia waishio jirani na saluni hiyo kufuatia huduma chafu za kuchukiza ambazo hufurahiwa na shetani na malaika wake tu.

Msamaria Mwema: Halooo.... halooo... jamani halooooo, hapo ni Makao Makuu ya OFM?
OFM: Ndiyo mama, tukusaidie nini?
Msamaria Mwema: Mna habari jamani?
OFM: Zimejaa tele, ila hata ya kwako inaweza kuwa bora kuliko tulizonazo.

Msamaria Mwema: Hapa Sinza Kwaremi (Dar) kuna saluni moja inaendesha vitendo vichafu vya ngono na hakuna sheria yoyote inayochukuliwa dhidi ya wahusika.

...Huyu alinaswa akikimbia baada ya OFM kutia maguu eneo la tukio.
OFM: Saluni ya ngono? Kivipi mama? Hebu fafanua tafadhali!
Msamaria Mwema: (kwa sauti ya juu mno) ninyi njooni mtajua kila kitu hukuhuku lakini inaendesha mambo ya ajabu (simu ikakatika).

OFM MZIGONI
Bila kupoteza sekunde, mkuu huyo wa MKT, aliwapanga ‘makamanda’ maalumu na kuwapa maelekezo muhimu ya jinsi ya kujua ukweli juu ya uovu uliodaiwa kutendwa kwenye saluni hiyo.

UCHUNGUZI
OFM iliwatuma vijana wake ‘watanashati’ hadi eneo lililotajwa ili wachunguze kama kweli kuna saluni yenye jina lililotajwa na mtoa habari wetu.

Baada ya maelekezo hayo, vijana hao wakiongozwa na roho safi ya kunyoosha maadili katika jamii, walifika hadi Sinza na kukuta saluni yenye jina hilo ambapo walianza kufanya upelelezi wa hali ya juu mno huku wakiwa makini kuliko hata neno lenyewe.

UTHIBITISHO
Baada ya kutinga eneo hilo, OFM iliendesha upelelezi maalumu kwa kuwauliza baadhi ya wakazi na watu wanaofanyia shughuli zao za kujiingizia riziki na kupata ukweli halisi juu ya ufuska ufanywao ndani ya saluni hiyo.

Katika uchunguzi huo, OFM ilipata uthibitisho kuwa kweli ibilisi yuko katika hesabu zake za mwaka kwa kufanya uchafu wa kufuru.
Ilielezwa kwamba, watumishi wa saluni hiyo ambao ni warembo, hujifanya wanatoa huduma ya kuchua mwili (body massage) kwa Sh. 25,000/= kwa vyumba na huduma za kawaida, lakini kwa vyumba vyenye choo na bafu kwa ndani (self contained) ni Sh. 35,000/=.

HUDUMA
Katika upelelezi huo, ilibainika kuwa mteja akilipia gharama ya vyumba vya self contained, ana uhuru wa kuchagua kama atapenda kufanyiwa huduma ya uchuaji kwa mikono tu au kwa matiti na wakati mwingine mwili mzima huku mtoa huduma hiyo akiwa amevua nguo zote!

Ikazidi kuelezwa kuwa, endapo mhudumiwaji atataka huduma hiyo ya mchuaji kuvua nguo zote, atafanyiwa hivyo lakini kama atazidiwa na kuhitaji huduma ya ngono, atatakiwa kuongeza Sh. 50,000/= kwa msichana huyo wa huduma na kufanya gharama kuwa zaidi ya Sh. 80,000/=.

“Wamekuwa wakifanya vitendo viovu sana, yaani ngono njenje, jamani hii siyo saluni, bali ni danguro la ngono fuatilieni mtangundua juu ya ukweli huu,” alisema mmoja wa raia katika upelelezi wa OFM.

OFM NDANI YA NYUMBA
Ili kujiridhisha na maelezo hayo, timu ya OFM ilituma vijana wake tofauti kwa muda wa siku tatu mfululizo na kubaini kuwa yote yaliyosemwa na kutajwa kwa kirefu yanatendeka ndani ya saluni hiyo!

‘Askari’ wa kwanza wa OFM aliingia ndani ya saluni hiyo (jina linavunda kwenye droo za meza yetu) na kuwakuta wahudumu wamejaa tele na alipowauliza juu ya huduma ya masaji na ngono, walijibu kwa sauti ya furaha na bashasha kubwa bila kujua kuwa kijana wetu alikuwa na vifaa maalumu vya kunasia sauti.

“Ni wewe tu jamani, kwani wewe ni mgeni maeneo haya? Mbona utaratibu unaeleweka, lakini maelezo ni hayo kwa hiyo karibu sana,” alisema mmoja wa warembo hao huku akilegeza macho mithili ya mgonjwa wa degedege.

Siku mbili zilizofuata, askari wa OFM waliendelea kupata stori na maelezo ya aina hiyohiyo.

MTEGO!
Siku ya tukio, (mwanzoni mwa wiki hii) OFM iliweka mtego kwa kumpeleka kijana wake ili ajifanye anahitaji huduma hiyo ya kufanyiwa masaji mwili mzima na baadaye ajifanye amezidiwa na kuhitaji huduma ya ngono.

Katika mtego huo, OFM ilitoa taarifa polisi ambapo ‘vijana wa IGP Ernest Mangu’ hawakulaza damu, wakatoa ushirikino wa kutosha kwa OFM.

MTEGO WAFYATUKA
Kama kawaida, OFM huwa haishindwi linapokuja suala la oparesheni maalumu kama hiyo, fuatilia sana. Mtego wake ulifyatuka ambapo mmoja wa vijana wake alijifanya kuhudumiwa (angalia picha ukurasa wa mbele).

Baada ya kuweka mazingira sawa, OFM na polisi wa kike na kiume walivamia na kufanikiwa kufuma laivu matukio mengi ya ufuska mkubwa (ukitaka kuona zaidi, unakaribishwa Bamaga ofisini kwetu).

WAUME ZA WATU!
Baada ya zoezi hilo kukamilika, baadhi ya mashuhuda (hasa akina mama) walisikika wakishukuru kufumuliwa kwa saluni hiyo kwa kuwa ndoa zao zilikuwa zimeanza kuota magugu kwani wateja wengi wa saluni hiyo ni waume za watu na vigogo serikalini!

“Jamani tunashukuru sana, waume zetu walikuwa wanakimbilia hapo, ugomvi kidogo tu, mwanaume anakwenda hapo na akirudi nyumbani hana habari kabisa na mkewe, safi sana OFM na polisi kwa jumla,” alisikika mama Joyce akishangilia kufumuliwa kwa saluni hiyo.

SOO POLISI
Baada ya ‘sheshe’ hilo, warembo sita walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa upelelezi maalumu.

MMILIKI
Katika upelezi wa awali, watumishi hao walimtaja mmiliki wa saluni hiyo kwa jina moja la Chifu huku wakishindwa kuweka wazi na kufafanua kwa undani zaidi.

KAMANDA WAMBURA UPO?
Gazeti hili lilifanya jitihada za hali ya juu kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ili azungumzie juu ya sakata hilo, lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

KUTOKA IJUMAA:
Timu nzima ya OFM na dawati la Ijumaa kwa jumla, tunalaani vikali kuwepo kwa vitendo viovu kama hivi vinavyokwenda kinyume na maadili na utamaduni wetu kwa sababu vinachochea mmomonyoko wa maadili na ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Source: GPL

kutoka kwa bibi,
Nami nawaunga mkono OFM kwa kazi nzuri ya kufichua maovu yanayofanyika ndani ya jamii. Waume zenu wakiwakatalia kwenda kufanya kazi kwenye masaluni haya mnanuna nakusema wanawanyima haki zenu. Haki zenyewe ni hizi? Acheni upuuzi kwani maradhi nayo ni mengi sana. Wajukuu zangu wa kiume, hasa ambao wake zenu, dada zenu wanafanya kazi kwenye masaluni hasa ya kiume hebu muwe mnafuatilia nyendo zenu. Wanapotea. Na muwe wakali kwelikweli.

Friday, July 19, 2013

KUKOPA SIO DHAMBI WAJUU ZANGU

                        Daima mbele mama


Sinta mjukuu wangu siku zote yanapoinuka mafanikio, vikwazo navyo huinuka. Usijali we fanya yako mama. Kukopa sio dhambi.

Ama kweli, binadamu hawana wema na kwa hakika mtu huwezi ukafanya jambo ukamfurahisha mwanadamu. Siku ngapi hizi mimi bibi yenu nilikuwa nimetulia na fimbo yangu haijachapa mtu kwa muda mrefu lakini kwa hili, aah!aah! nimejikuta nashindwa kujizuia na kuchukua bakora yangu ili niwacaharaze kisawasawa wale wote wenye tabia kama hii ili wajifunze.
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kudharau wenzao na kuwakashifu kuwa wana maisha ya hali ya chini na wao kujiona kuwa wapo matawi ya juu. Sawa, kama Mwenyezi Mungu akujalia wewe maisha bora, ni heri na Mshukuru sana kwa hilo na waombee wote walio katika hali duni siku moja Mwenyezi Mungu nao awajaalie. Lakini usitumie umasikini wa mtu kama fimbo ya kumchapia kwani kumbuka kuwa aliyekupa wewe ndie aliyemnyima yeye na dunia ni duara ipo siku unayemdharau atapanda juu na wewe ukashuka chini. Mmh!Hapo sasa. 
Mwanadada wa watu mlikuwa mkizonga kuwa ooh! anaishi maisha ya chini kwani anaishi uswahilini, gari lake ni la bei nafuu sijui kiberiti, mara ooh!ni mzee, hivi hebu kwanza niwaulize, kuwa mzee ni dhambi? Na ni nani ambaye atabaki kijana milele? Nawaambieni nyoote hata muwe na urembo wa kiasi gani, kuzeeka ni lazima. Tena kwanza kuzeeka kwa sasa ni bahati. Vijana wengi wanakufa wakingali wadogo.
Nikirudi kwa upande wa ridhiki, kila mtu hupata kwa wakati wake na imepangwa kwa mafungu, leo kwako na kesho kwa mwenzako. Na pia, si kwamba ukipata basi ndio iwe matangazo dunia nzima. Mwanamke mwenye stara hufanya mambo yake kimyakimya na watu hubaki kujionea wenyewe.
Mlimsema mjukuu wangu sana kwamba maisha yake ni ya chini kumbe hamkujua kuwa mjini mipango na kila mtu na kichwa chake, dada wa watu kajipanga kafungua duka lake tena kwa suprise, mmeibuka eti ooh!kafungua kwa fedha za mkopo mmh!Kweli binadamu hawana jema na siku zote hupenda kuona wenzao wapo chini na wao peke yao ndio wawe juu. Lakini wanasahau kuwa mgawa ridhiki ni allah pekee. Hivi aliyewaambia kuchukua mkopo ni dhambi nani? Kwanza mtu ukipewa mkopo ujuwe wewe upo juu na unaaminika kwani mkopo hautolewi hovyo hovyo tu kwa kila anayeomba katika mabenki. Vipo vigezo ambazo vinaangaliwa ili mtu upate mkopo. Kama ni rahisi hebu kajaribu na wewe uone kama utapewa. Na halafu dunia ya leo, kila mmoja anakopa. Kula yetu, lala yetu na hata biashara zetu, mitaji ya wengi imepatikana kwa njia ya mkopo.
Kwahiyo mjukuu wangu, kama umekopa, au hukukopa wewe fanya yako na waache wao povu la mdomo liwatoke. Nchi yenyewe inakopa au wao hawalijui hilo sembuse wewe? Bibi fanya yako wee! Kopa, ukiona hautoshi kopa tena kadri uwezavyo kikubwa unalipa deni lako.Kwani mabenki, Mabaypot, sijui black na mapride yameletwa kwa ajili gani? Yameleletwa ili kuinua wananchi hasa sisi akina mama. Mimi mwenyewe bibi yako kibanda changu nimejenga kwa fedha ya mkopo halikadharika ada za wanangu.
Na sasa bakora inahamia kwa watumishi wote ambao wanatabia ya kutoa siri za ofisi wanazofanyia kazi kwa manufaa yao binafsi. Mtumishi anayejua vema maadili ya kazi yake kamwe hawezi kutoa siri za ofisi hasa za wateja wa ofisi anayofanyia kazi kwani ni kosa sana. Lakini hili liwe funzo kwa waajiri kuwa makini na watumishi wanaowaajiri katika makampuni yao kwani wengi wao sasa hawana maadili ya kazi. Kwa mtu anayeyajua vema maadili ya kazi yake, na ameapishwa, sijui kama makampuni mengine hasa binafsi yanafanya hivyo lakini kwa sisi watumishi wa umma tunaapishwa na ikigundulika mtu ametoa siri za ofisi hatua kali za kinidhamu huchukuliwa dhidi yake. Hivyo mtumishi atakayebainika kutoa taarifa za kiofisi za mwanadada inayesemekana alikopa katika kampuni fulani achukuliwe hatua za kisheria kwani amemdhalilisha mteja na ofisi yake.