Monday, June 3, 2013

UKISTAAJABU YA MUSA...........................


SHAME UPON YOU WOMAN!!!



Picha kwa hisani ya www.sintah.com
Wajukuu zangu, katika pitapita zangu ndani ya mitando na blog mbalimbali, leo nimeona kituko cha ajabu sana. Nilikutana na picha hiyo hapo juu na ghafla bibi yenu mie nikajisikia damu ikinichemka na kichwa kikanivimba kwa hasira. Nikajiuliza hivi huyu dada hapo juu ana akili zake timamu au ana upungufu kidogo kichwani? Hata kama ndio mnasema mnakwenda na wakati wajukuu zangu, ndio hivi? Eeeh!Kuvaa uchi ndio kwenda na wakati? Hebu ifikie wakati mkawa na aibu machoni mwa watu. Sifa ya mwanamke ni kujisitiri bwana. Kweli mdada mzima na akili zako timamu unaweza kuanika matako yako nje kiasi hiki?Samahanini kwa kutumia lugha hiyo kali lakini yote hii ni sababu ya hasira niliyonayo juu ya kitendo hiki. Mmh!Una wazazi kweli wewe?Una ndugu kweli wewe? Yaani sielewi hata niseme nini kwakweli maana bibi yenu leo nimekuwa mdogooo kama piriton. Kweli kuna watu makauzu hapa duniani.
Kutoka moyoni mimi bibi yenu kitendo hiki kimenichafua mno kwani kinatudharirisha wanawake kwa ujumla.
Kifupi nawasihi sana wajukuu zangu tujihifadhi. Zipo nguo nzuri tu za out za kisasa ambazo zinamuhifadhi mwanamke  ambazo anaweza kuvaa na akaonekana ni wa kisasa lakini sio hivi ndugu zangu.