Ilikua ni mida ya saa tatu asubuhi. Mimi bibi yenu nilikua ofisini katika harakati za kujitafutia ridhiki. Siku hiyo nilikua kwenye kikao. Lakini nikiwa katika kikao hicho, simu yangu ya mkononi iliita. Nilipoiangalia screen ya simu yangu, niliiona namba ya babu yenu. " Sijui anasemaje huyu mzee mwenzangu". Nilijisemea mwenyewe huku nikiinuka na kutoka nje ili nikamsikilize mpenzi wangu. Nilitoka taratibu kwa mwendo wa kunyata ili nisiwasumbue wajumbe wenzangu waliokuwemo katika kikao hicho. Nilifika nje na kupokea simu ya babu yenu haraka haraka kabla haijakata kwa sababu ilikua imeita kwa muda mrefu. Nilipopokea simu, babu yenu alinieleza kuwa, eti kuku wangu ninayempenda sana amepigwa na jiwe mguuni na watoto hivyo ameumia na anatembea kwa kuchechemea.
"Mmh!Mume wangu bwana, yaani kanitoa kwenye kikao mbiombio kumbe jambo lenyewe alilotaka kuniambia ndio hili? Nilijikuta nikiongea peke yangu mara baada ya kumaliza kuongea na simu ile. Basi, niliamua kurudi ukumbini kuendelea na kikao. Lakini kabla sijapiga hatua nyingi, nilisikia sauti ya mwanamke ikiita nyuma yangu " Bibi!Bibi!" Niligeuka nyuma kumwangalia huyo aliyekua akiniita. Alikua ni mwanamke apata miaka thelathini hivi. Mwanamke huyu alikuwa ameongozana na watoto wadogo wapatao watano na mwingine mdogo alikua amembeba mgongoni. Yeye pamoja na watoto wale walionekana wamechakaa. Kwa kuwatazama tu, ilionyesha dhahiri kwamba, walikuwa wakiishi maisha ya shida. Wale watoto wadogo watano kila mmoja alikuwa ameshika kipande cha muhindi mkononi na yule wa mgogoni alikuwa anakula kitumbua. Nilisimama kumsikiliza mwanamama huyu.
"Shikamoo bibi". Aliniamkia mwanamama wa watu kwa adabu.
"Marahabaa, hujambo?".
"Sijambo bibi. Faraja, mwamkieni bibi'. Yule mama aliwaamuru watoto aliokuwa ameongozana nao waniamkie.
"Shikamoo". Waliniamkia wote kwa pamoja.
"Marahabaa watoto wazuri, hamjambo?".
"Hatujambo".
"samahani bibi, nina shida ya kuonana na Afisa Maendeleo ya Jamii kwani nimeelezwa kuwa yumo ukumbini kwenye kikao". Mama yule aliniambia.
"Ni kweli yumo lakini hawezi kutoka kwani yupo kwenye kikao. Njoo kesho".
"Hapana, ni lazima nionane nae leo kwa sababu nina shida sana na ninahitaji msaada wake". Mwanamama yule aliniambia huku akionyesha hali ya kukata tamaa. Kama mzazi nilijikuta naingiwa na huruma na kumvuta pembeni ili kumdadisi zaidi.
"Kwani mwanangu una tatizo gani?'. Nilimwuliza kwa upole. Lakini badala ya kunijibu mama huyu analengwalengwa na machozi ambayo yanatengeneza vijito viwili na taratibu yanabubujika kwa wingi.
"Aa!Aaah!Hapana. Usifanye hivyo, acha kulia mwanangu. Tulia unieleze tatizo ni nini ili niweze kukupa ushauri wa nini cha kufanya. Mama wa watu alishika upindo wa khanga yake iliyokua imechakaa na kujifuta machozi yake. Watoto wake walikua pembeni wakicheza wala hawana habari nae.
"Mmh!Haya nieleze mwanangu, nini tatizo?".
"Mh!Bibi yangu, mimi nina shida kweli. Hivi unavyotuona, mimi na watoto wangu hatujala tangu jana. Njaa inatuuma kweli".
"Hamjala tangu jana?".
"Ndio".
"Tatizo nini, una mume?'. Nilimwuuliza
"Mmh!Bibi yangu, mume ninaye na tena tumefunga ndoa ya kanisani. Lakini ni mume jina tu bibi yangu. Mume amekuwa haeleweki. Hivi sasa yapata miezi minne hajatia mguu nyumbani".
"Ati?".
"Nakwambia bibi, huu ni mwezi wa nne mume wangu hajatia mguu nyumbani. Wala sijui yupo wapi?".
"Mmh!Makubwa. Haya, tatizo ni nini?
"Pesa". Alinijibu kwa mkato mama yule
"Pesa? Unamaanisha nini?". Nilimuuliza ili anifafanulie kwa sababu kiukweli sikuwa nimemuelewa anamaanisha nini?.
"Sisi huwa tunalima tumbaku. Kilimo cha tumbaku ndio huwa shughuli yetu kuu. Na mimi ndio trekta lake.
"Wewe ndio trekta lake? Kivipi?".
"Mimi ndio hufanya shughuli zote za shamba kuanzia kuandaa mashamba, kuandaa mbegu, kupanda, kutia mbolea yaani bibi shuguli zote ni mimi hadi tumbaku inakua tayari kwa kwenda sokoni. Hapo yeye ndio utamwona anajileta na kujidai usimamizi wa uuzaji wa tumbaku. Wakati wa kulima yeye shamba humwoni. Kutwa kuchwa, yupo kwenye kahawa na kucheza bao. Ndio kazi anayoiweza.
"Maskini". Nilijikuta nikijisemea mwenyewe.
"Hela ikitoka sasa, humwoni nyumbani hadi fedha zitakapomwishia ndio unamwona anarudi nyumbani bila ya sukari wala chumvi mkononi. Kusema ukweli, mimi nimechoka kufanywa mtumwa. Mwanaume ajui watoto wanakula nini wala wanavaa nini?. Akipata pesa, anatafuta na wanawake wengine wa kumsaidia kuzitumia ilihali mimi na watoto tunaadhirika jamani, iiiiiiiiiiiiii!'. Mama yule aliangusha kilio tena kwa uchungu.
"Aah!Nyamaza bwana. Jikaze haya ni maeneo ya kazi. Watu watakushangaa. Umesikia mwanangu, jikaze". Baada ya kumbembeleza kwa muda mama wa watu alinyamaza na kutulia.
"Sasa, ulikua unamtafuta Afisa Maendeleo ya Jamii ili akusaidie nini?". Nilimwuliza kwa mtego ili kuona upeo alionao katika hili.
"Baada ya kuniona nahangaika sana, kuna jirani yangu mmoja aliniambia kuwa nije kwenye ofisi ya Maendeleo ya Jamii nimwone Afisa Maendeleo ya Jamii nimwelezee matatizo ili wamwite na kuongea nae".
"Ni kweli, Afisa Maendeleo ya Jamii ana uwezo wa kumwita na kumtaka atimize wajibu wake kama baba katika familia. Hivyo kuwa na uvumilivu ili akitoka kwenye kikao uonane nae. Usijali, atakusaidia, sawa?.
"Kwani kikao kinatarajiwa kuisha saa ngapi?". Aliniuliza
"Bado kidogo, nadhani baada ya kama dakika arobaini hivi".
"Sawa, ngoja nivumilie. Yaani hata kama atatoka saa kumi, niko radhi kumsubiri".
"Sawa, yatakwisha tu". Nilimtia moyo.
Baada ya mazungumzo haya, nilimpa shilingi elfu mbili ili awanunulie watoto chakula wale katika mgahawa wa kazini kwetu. Mama yule alishukuru sana na kuniombea dua nyingi sana kwa Mwenyezi Mungu. Nilimwacha mama yule na kurudi kwenye kikao. Lakini kwa muda wote niliokaa kikaoni, sikua na raha kabisa. Kila nilipomkumbuka mwanamama yule kifua kilinifura kwa hasira na kwa kua Mwenyezi Mungu alinijalia busara na uwezo mkubwa wa kuandika kwani kabla ya kuingia katika kazi hii ninayoifanya sasa, mimi bibi yenu niliwahi kufanya kazi ya uandishi wa habari katika chombo kimoja cha habari, hivyo niliona ipo haja ya kuongea na kuwacharaza bakora Watoto na Wajukuu zangu wa kiume kwa njia ya kalamu. Basi niliporudi nyumbani tu siku hiyo nilichukua kalamu na karatasi na kuanza kuwacharaza vijana wangu kama ifuatavyo:
Kwa watoto na wajukuu zangu wooote wa kiume,
Salamu sana. Natumaini mu wazima wa afya njema. Mtakapo kujua hali yangu mimi bibi yenu ni mzima wa afya njema. Hofu kwenu ninyi.
Dhumuni hasa la barua hii ni kuongea nanyi watoto na wajukuu zangu wa kiume. Hivi nyinyi vijana mmechanganyikiwa? Nawauliza tena, mmechanganyikiwa? Kusema ukweli, nakerwa sana na hii tabia yenu ya kuwa mnazalisha wanawake na kuwatelekeza wao pamoja na watoto wao. Kama unajiona bado hujakomaa na bado huna uwezo wa kuweza kumudu familia ni kwanini unaoa, kwanini unafuata binti wa watu unampachika mimba halafu unamtelekeza? Unataka nani akulelee watoto wako? Yaani raha zako mwenyewe halafu unawapa kero wengine, hivi ninyi mna wazimu. Tena nyie ndio chanzo kikubwa cha tatizo la watoto wa mitaani. Yaani napatwa na hasira natamani kama niwe nawaona hapa mbele yangu ili niwacharaze bakora hasa.
Jamani, hivi kweli mwanaume mzima, unaamka na kwenda kukaa kwenye kahawa siku nzima kuanzia mawio hadi machweo na una mke na familia unakutegemea. Haya, shughuli za kujipatia kipato unazifanya saa ngapi? Yaani mkeo ndio anahangaika na shuguli za kujua familia itakula nini wewe baba upo upo tu, hivi huoni aibu?
Na wababa wengine wanazalisha wanawake kisha wanawatelekeza na tena wanaume wengine wana uwezo tu ila eti kwa sababu kapata mwanamke mwingine basi damu yake ya awali anaisahau kabisaa tena anajifanya kama vile hajawahi kuzaa. Anaponda raha tu.
Mimi bibi yenu nasema nakereka sana na tabia hii kwani tabia hii imeota mizizi sana katika dunia hii ya leo. Nawataka mbadilike na mbebe majukumu yenu kama mababa wa familia. Wengine inafikia mahali wakiwaona wake zao au wazazi wenzao wanabadilisha njia ili wasionane nao kwa kuogopa watawaomba hela ya matumizi. Nawaeleza raha ya dunia ni watoto hivyo tunzeni watoto wenu kwa kadri ya uwezo ambao Mungu amewajalia. Kukimbia si suluhisho kwani damu yako ni yako tu na aibu ni yako.
Na wapo wengine hukataa kutunza watoto wao wakabaki wakiponda raha tu halafu wakizeeka na kufikia umri kama wa mimi bibi yenu ambapo wanakua wamefulia ndio memory inawarudia kuwa walizaa mahali fulani na kuanza kutafuta watoto wao kwa njia mbalimbali za mawasiliano kama vile radio, runinga nk. Nawauliza, kama wewe hukumtunza mtoto alipokua mdogo unamtafutia nini uzeeni. Mmh! Mama kahangaika kulea mwanae kwa kufanya ujasilimali na kusomesha mwanae na sasa ana kazi nzuri ndio unajileta nasema mshindwe kwa jina la bwana.
Mimi bibi yenu nasema acheni tabia hizo. Nataka kila mmoja abebe majukumu kama baba na hiyo ndiyo sifa ya mwanaume mwenye akili timamu. Nataka mama abebe majukumu ya umama na baba abebe majukumu ya ubaba.
Kwa leo naishia hapa. Tuonane tena kwa mada ijayo.
Mimi bibi yenu,
Thereza.
www.kifimbochabibi.blogspot.com

No comments:
Post a Comment